Dondoo

Buda afokea kicheche aliyemtia presha ateme mkewe ili amuoe

January 4th, 2024 2 min read

MTWAPA MJINI

Na JANET KAVUNGA

JAMAA wa hapa alimkemea mpango wake wa kando, mwanadada alipomtaka amtaliki mkewe ili amuoe.

Kalameni amekuwa akitoka na mwanadada huyo kwa muda, uhusiano ambao umekuwa wa siri.

Juzi, demu alimpa takwa ambalo lilimfanya jamaa kulipuka kwa hasira kwa kumwambia wakati wa kupeleka uhusiano wao hatua nyingne umefika.

“Nimekuwa nawe kwa miaka mitatu sasa na ni wazi kuwa mkeo hakupi raha ninavyokupa.

“Mtaliki sasa unioe niendelee kukukoleza mapenzi na raha tele,” demu alimwambia jamaa lakini akajuta kutoka takwa hilo.

“Sikiza mwanadada,hauwezi kufikia mke wangu kwa hali zozote na kama unafikiria ninaweza kumuacha au nikuoe unaota,” jamaa alifoka na demu akaingiwa na baridi.

***

Mdada asutwa kwa kudai michepuko inampa raha

BOMBOLULU, MOMBASA

Na JANET KAVUNGA

MDADA wa hapa aliungama kuwa michepuko huwa inampa raha na kumfanya akate kiu Y a uroda akisema shughuli za chumbani akiwa na mkewe zimekuwa mazoea.

“Sio siri mimi huchangamkia michepuko kwa kuwa inanifanya kupata raha kwa kuwa nimezoeana sana na mume wangu. Ninagawa asali mara moja kwa mwezi na kusema kweli huwa ninafurahia,” demu alieleza wenzake katika mjadala mkali kuhusu iwapo mwanamke aliyeolewa anafaa kuwa na mipango ya kando na athari za kugawa asali nje ya ndoa.

Hakuna aliyemuunga mkono mwanadada huyo na akaonywa kuwa anaweza ndoa na afya yake kwenye hatari.

***

Janadume lililoleta mke wa pili kimasomaso lazabwa kofi na mkewe

MATUU MJINI

NA JOHN MUSYOKI

KISANGA kilishuhudiwa kwenye steji ya magari mtaani hapa, mwanadada alipomkabili mumewe kwa kuwasili akiwa na mke wa pili.

Demu alifika steji kumlaki mumewe kutoka jijini jamaa aliposhuka gari akiwa na mwanamke mwingine. Cha kushangaza ni kuwa jamaa hakusita kumtambulisha demu huyo kama mke wa pili.

Hapo ndipo mke wa kwanza alipolipuka na purukushani ikaanza.

Demu alimrukia mumewe na kumzaba makofi huku akidondokwa na machozi.

“Wewe ni mwanaume sampuli gani? Ulikwamilia jijini muda huo wote kwa sababu ulikuwa na mke wa pili. Hata huna aibu kuniambia ni beib yako. Kama hunitambui kama mkeo nyumbani hukanyangi ng’o,” mke aliwaka.

Ilibidi wawili hao kutenganishwa na jamaa, na demu wakaenda zao.