Buffa Otieno abwaga Tundo kuwa mwanamichezo bora nchini wa Oktoba

Buffa Otieno abwaga Tundo kuwa mwanamichezo bora nchini wa Oktoba

Na AGNES MAKHANDIA

NYOTA wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande Alvin Otieno ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa LG/SJAK.

Otieno maarufu kama Buffa, kutokana na nguvu zake za kukabili wapinzani kama nyati, alizawadiwa runinga ya inchi 55 ya UHD LG inayogharimu Sh105,000 sokoni.

“Nafurahi sana kupokea zawadi hii. Nimeipata, hasa baada ya kupona jeraha na kushuhudia mchezo wangu ukiendelea kuimarika. Bado nalenga juu na pia naomba wachezaji wote wajizatiti,” alisema Buffa aliyeandamana na Kocha Mkuu wa timu hiyo maarufu kama Shujaa, Innocent ‘Namcos’ Simiyu, nahodha Nelson Oyoo na afisa kutoka Shirikisho la Raga Kenya (KRU) Ian Mugambi katika klabu ya michezo ya Parklands hapo Novemba 19.

Buffa alichangia pakubwa katika Shujaa kushinda tuzo ya Safari Sevens kwa mara ya kwanza tangu 2016 mwezi uliopita ugani Nyayo.

Mwanafunzi huyo wa zamani wa Shule ya Upili ya Kakamega High aliyejiunga na mabingwa wa Ligi Kuu nchini (Kenya Cup) KCB kutoka Homeboyz majuzi, alilemea bingwa wa Mbio za Magari Afrika Carl Tundo, mshindi wa Kombe la Dunia mbio za milimani Joyce Njeru, mabingwa wa Paris Marathon Elisha Rotich na Angela Tanui pamoja na bingwa wa New York Marathon Joyceline Jepkosgei na mchezaji wa mpira wa vikapu Byron Mabonga kutoka klabu ya Ulinzi Warriors.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

You can share this post!

Isuzu EA yaongeza mkataba na gunge Eliud Kipchoge kwa miaka...

Njaa ilivyouza magaidi

T L