Habari Mseto

Bunge la Kaunti ya Trans Nzoia lafungwa

October 20th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Bunge la Kaunti ya Trans Nzoia lilifungwa kwa muda baada ya watu wawili kupatikana na virusi vya corona Jumanne.

Karani wa bunge hilo Ainea Indakwa aliagiza wafanyakazi wote kusalia nyumbani kwa muda wa siku 14 kulingana na maagizo ya Wizara ya Afya.

Bw  Indakwa alisema ni jambo la kusitisha shughuli za bunge mara moja . “Bunge hilo litabakia kufungwa kwa muda wawiki mbili kuanzia Oktoba 19.lakini tutatoa huduma za mitandaoni,” alisema.

Aliwaomba maafisa wa bunge hilo wake nyumbani,waoshe mikono na wavae maski huku wakizingatia umbali wa mita moja.

Wakati huo huo kilabu kimoja mjini Kitale kimefunga kwa  muda mfupi baada ya visa vya corona kuongezeka Tran Nazoia.