Habari Mseto

Bunge la Zimbabwe lasitisha vikao

July 27th, 2020 1 min read

By KITSEPILE NYATHI

Bunge la Zimbabwe limesitisha vikao vyake baada ya wabunge wawili kupatikana na virusi vya corona.

Spika Jacob Mudewnda alisema Jumatatu kwamba wabunge hao wawili walikuwa kati ya kamati iliyotembelea mji wa Gweru Magharibi Kusini mwa mji Harare.

Dereva wa basi na mwanahabari aliyesafiri pamoja kwenye safari hiyo pia walipatikana na virusi vya corona.

“Kukatizwa kwa shughuli za bunge kunaturuhusu kutakasa jengo lote na kuosha ili tuwe na usalama wa wabunge wetu an maafisa wetu na umma,” Bw Mudenda alisema kwenye ilani.

Nchi hio imekua ikishuudia kuongezeka kwa virusi vya corona na vifo.

Visa vya corona vimeongezeka mara dufu hadi 2,512 Jumapili huku vifo vikifikia 34.

Zimbambe imesitisha kufunguliwa kwa shule tangu zifungwe mwezi Machi tangu kuzuka kwa virusi hivyo vya corona.

Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita aliweka kafyu ya usiku hadi asubuhi ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.