Habari Mseto

Bwanyenye wa Thika aliyetoweka bado asakwa

October 4th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Uchunguzi bado unaendelea kumsaka mfanyabiashara maarufu wa mjini Thika ambaye alipotea Septemba 21 huku swala la alipotowekea likizua utata.

Kulingana na mplelezi mkuu wa operesheni hiyo  Bw John Kanda, taarifa sita tayari zimerekodiwa kwamba Bw Gitau alitekwa nyara ama alipanga kupotea kwake.

Pia kuna uwezekano kwamba Bw Gitau alijitia kitanzi labda kwa kujirusha mtoni kwani kuna ujumbe ulikuwa kwa gari lake uliosema kwamba alikuwa anwazia kujitia kitanzi kufuatia biashara zake kudorora wakati wa msimu wa corona.

Wapelelzi walisema kwamba Bw Gitau alionekana mara ya mwisho kwenye hoteli ya Bluepost saa nne asubuhi kabla ya kutoweka.

“Si rahisi iwe alijirusha ndani ya mto Chania kwani watu wengi wangekuwa wameshuhudia akijirusha,”alisema Bw Kanda.

Bw Kanda ambaye ni mkuu wa DCI kaunti ndogo ya Gatanga alisema kwamba wake zake watatu wa Bw Gitatu dungu zake, dereva wake na mkurugenzi mkuu wa biashara zake walirekodi taarifa.