Habari Mseto

Bwawa Uhuru latapika maji na kuathiri baadhi ya wakazi wa Ruiru

December 5th, 2019 1 min read

Na MWANDISHI WETU

BWAWA Uhuru lililopo mjini Ruiru limetapika maji Alhamisi asubuhi kutokana na mvua iliyopitiliza.

Wakazi wa mtaa wa Varsityville eneo la Kamakis wameathirika kukiwa na ripoti kwamba maji yameingia katika baadhi ya nyumba.