Caf: Maswali tele kuhusu maandalizi ya Tusker, Gor

Caf: Maswali tele kuhusu maandalizi ya Tusker, Gor

Na CECIL ODONGO

KWA mara nyingine timu za Kenya zimefeli kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Mashirikisho hali hiyo ikizua maswali kuhusu maandalizo yanayochangia rekodi duni katika CAF.

Mnamo Jumapili mibabe wa soka nchini Gor Mahia na Tusker walibanduliwa kwenye raundi ya pili ya Caf na AS Otoho d’Oyo ya Congo Brazzaville na CS Sfaxien ya Tunisia mtawalia.K’Ogalo ilienda sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya AS Otoho d’Oyo katika uga wa kitaifa wa Nyayo.

Kwa kuwa ilichapwa ugenini, Gor ilihitaji ushindi wa 2-0 kutinga hatua ya makundi au 1-0 kulazimisha mechi hiyo iamuliwe kupitia mkwaju wa penalti.Tusker nao waliangukia pua baada ya kulemewa 1-0 na CS Sfaxien mnamo Jumapili usiku.

Mvamizi Aymen Harzi alifunga bao hilo kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 34 kuzamisha zaidi chombo cha Tusker. Beki Kevin Monyi naye alilishwa kadi nyekundu zikiwa zimesalia dakika 10 mchuano huo ukamilike.Huu sasa ni msimu wa tatu ambao Kenya itakosa timu katika hatua ya makundi kwenye Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Mashirikisho.

Mara ya mwisho Kenya ilikuwa na timu kwenye makundi ni msimu wa 2018/19 ambapo Gor ilipiga hatua na kutinga robo fainali ila ikabanduliwa na RS Berkane ya Morocco kupitua jumla ya magoli 7-1.Tangu wakati huo, Gor imebanduliwa katika raundi ya pili na DC Motema Pembe(2019/20), Napsa Stars (2020/21) na sasa AS Otoho d’Oyo (2021/22).

‘Hatukuwa na kikosi cha kutosha. Inasikitisha kuwa tulikuwa na wachezaji 16 pekee kwa mechi muhimu kama hii. Sasa itabidi tujipange ila ni vigumu kuwa tunayaaga mashindano haya japo nilikuwa na imani tungetamba na kufika makundi,’ akasema Kocha wa Gor Mark Harrison.

Masaibu ya Tusker nayo yalionekana kuanza pale timu hiyo iliwatimua wachezaji 14 ambao waliwasaidia kushinda ligi na kuwasajili wengine wapya.Aidha rekodi duni ya kocha Robert Matano dhidi ya timu kutoka Kaskazini mwa Afrika ilichangia kubanduliwa kwao.

Wanamvinyo hao waliibandua AS Arta Solar 7 ya Djibouti 4-1 kwenye mchujo ya klabu bingwa ila ikalemewa 5-0 na Zamalek ya Misri katika raundi ya kwanza ndipo wakaporomoka hadi kombe la mashirikisho.

You can share this post!

Gozi la wazito Inter, Real Uefa

Chager aashiria kushindwa

T L