Habari Mseto

Carrefour yabisha Westlands

April 24th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Duka la rejareja la Carrefour, limefungua tawi Westlands. Duka hilo lilifunguliwa lilipokuwa duka la Uchumi.

Lakini litakuwa hapo kwa muda tu kwani linatarajiwa kuhamia Sarit Centre.

“Nafasi tunamohudumia ni ya muda, tutahimia katika tawi jipya Sarit Centre ujenzi ukikamilika baadaye mwaka huu,” alisema meneja wake Kenya Franck Moreau.

Duka hilo linalenga kuchukua nafasi ya 5,000 mita mraba ili kuendesha operesheni zake vyema.

Wakazi wa Peponi, Kabete, Kitisuru, Kileleshwa, Kinoo na wanaoishi Waiyaki Way, Westlands, Riverside na Parklands watanufaishwa na huduma za duka hilo.

Hilo ni duka la pekee la Carrefour lililo karibu na katikati wa Jiji la Nairobi. Maduka mengine yamo The Junction, na Thika Road Mall.