Michezo

Casillas asema amepata afueni bada ya kulazwa hospitalini

May 9th, 2019 1 min read

JOHN ASHIHUNDU NA MASHIRIKA

LISBON, Ureno

Kipa matata, Iker Casillas wa FC Porto amewahakikishia mashabiki wake kwamba afya yake imeanza kuimarika baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo mapema juma hili.

Mlinda lango huyo alipatwa na tatizo hilo alipokuwa mazoezini na wenzake kabla ya kukimbizwa hospitalini kwa matibabu Zaidi.

Tayari wengi walikuwa wamemtumia poke kipa huyo wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania wakimtakia nafuu ya haraka.

Lakini baada ya kutibiwa aliwatumia mashabiki na wenzake ufueni kuwafahamisha kwamba kila kitu kipo shwari.

Casillas anakumbukwa kwa kuisaidia Madrid kutwaa mataji ya UEFA katika misimu 16, huku akiiwezesha nchi yake kunyakuwa Euro 2008 na 2012 pamoja na Kombe la Dunia la 2010.