Cavani apigwa marufuku na kutozwa faini ya Sh14 milioni kwa utovu wa nidhamu

Cavani apigwa marufuku na kutozwa faini ya Sh14 milioni kwa utovu wa nidhamu

Na MASHIRIKA

MFUMAJI Edinson Cavani wa Manchester United amepigwa marufuku ya mechi tatu na kupigwa faini ya Sh14 milioni kwa ujumbe wa kiuchochezi na wa matusi aliouandika kwa Kihispania na kupakia kwenye mtandao akaunti yake ya mtandai wa kijamii.

Nyota huyo raia wa Uruguay alikiri kosa lake aliposhtakiwa na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) mnamo Disemba 17 kwa matumizi ya maneno ambayo katika baadhi ya miktadha, yangefasiriwa kuwa na ujumbe kukosea walengwa heshima.

Cavani alipakia ujumbe huo mtandaoni baada ya kufunga bao la ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Novemba 29, 2020.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain (PSG) alifuta ujumbe huo pindi baada ya ‘uchochezi’ na ‘matusi’ katika baadhi ya maneno aliyotumia kubainika.

Zaidi ya marufuku na faini, Cavani atatakiwa pia kukamilisha kozi ya ana kwa ana ya mafunzo kuhusu nidhamu.

Kutekelezwa kwa marufuku dhidi ya Cavani kunaanza mara moja, hatua ambayo kwa sasa itamweka mwansoka huyo nje ya mechi ya EPL dhidi ya Aston Villa leo Januari 1, 2021.

Nyota huyo wa zamani wa Palermo na Napoli atakosa pia mechi ya nusu-fainali ya Carabao Cup itakayowakutanisha Man-United na Manchester City mnamo Januari 6 na mchuano wa raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Watford mnamo Januari 9, 2021.

You can share this post!

Amerika yamshutumu Rais Museveni kunyanyasa Wine

Shule zinapofunguliwa tuwe waangalifu Covid-19 isitulemee...