CECIL ODONGO: Uhuru kama mwenyekiti azungumzie siasa na misukosuko iliyopo Azimio

CECIL ODONGO: Uhuru kama mwenyekiti azungumzie siasa na misukosuko iliyopo Azimio

NA CECIL ODONGO

TANGU aondoke afisini baada ya muda wake wa kuhudumu kama Rais kukamilika, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amesalia kimya na kuonekana kupatanisha makundi pinzani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pamoja na eneo la Tigray, Ethiopia.

Hii ni licha ya kwamba muungano aliokuwa akiongoza wa Azimio la Umoja unakumbwa na maasi ya ndani hasa kufuatia madai kuwa wabunge wa Jubilee, cha Bw Kenyatta, kwamba wanaelekea mrengo wa Kenya Kwanza.

Katika kikao cha wabunge wa Azimio mnamo Jumanne, wengi wa wabunge wa Jubilee hawakuwepo.

Pia hawachakumbatia wazo la vinara wa muungano huo kuandaa maandamano dhidi ya serikali.

Ndiyo, Bw Kenyatta amestaafu kama kiongozi wa Kenya ila hilo halimaanishi hawezi kuzungumzia masuala ya kisiasa nchini na kuwa tu balozi wa kupatanisha viongozi wa nchi mbalimbali ambao wana uhasama wa kisiasa Afrika.

Kuna Marais wastaafu Afrika ambao kwa njia moja au nyingine wanaendelea kusimamia vyama na kutoa mwelekeo kwa miungano ambayo walikuwa wakisimamia wakiwa mamlakani.

Kwa hivyo, si vibaya iwapo hata Bw Kenyatta ataendelea kujihusisha na siasa na kukosoa serikali ya Rais William Ruto inapokosea au kukiuka ahadi ilizotoa kwa raia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

Wanasiasa ambao wapo kwenye mrengo wa serikali nao hawastahili kuona kujihusisha na Bw Kenyatta katika siasa za nchi kama njama ya kuhujumu utawala wa sasa.

Kuhusu Azimio, Bw Kenyatta anafaa ajitokeze na kuelezea wazi iwapo anaunga mkono mwelekeo ambao muungano huo unachukua kuhusu masuala mbalimbali.

Kustaafu urais si kizuizi cha kushiriki siasa za nchi na kukosoa uongozi uliopo mamlakani.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Tufufue BBI na kukumbatia mazuri...

KIPWANI: Katoi wa Tabaka alivyosalia na ‘baby...

T L