CECIL ODONGO: Viongozi wa Mulembe hawafai kumlaumu Raila kwa matatizo ya eneo hilo

CECIL ODONGO: Viongozi wa Mulembe hawafai kumlaumu Raila kwa matatizo ya eneo hilo

NA CECIL ODONGO

Mnamo Jumatatu, Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetang’ula pamoja na wanasiasa kutoka eneo la Magharibi waliandaa kikao na wanahabari ambapo walidai kuwa Raila Odinga amekuwa akitumia jamii ya Waluhya kisha kuitelekeza baada ya kila uchaguzi.

Huku wakirai jamii hiyo impuuze Bw Odinga kisiasa, Mabw Mudavadi na Wetang’ula waliorodhesha baadhi ya ‘madhila’ waliyodai waziri huyo mkuu wa zamani ameitendea Waluhya.

Walimhusisha Bw Odinga na sakati ya cheti cha masomo kinachomwandama Seneta wa Nairobi, Johnson Sakaja na ODM kukosa kumpa Tim Wanyonyi ambaye ni nduguye Wetang’ula tikiti ya kuwania ugavana wa Nairobi.

Isitoshe, walidai baada ya ‘handisheki’, Bw Odinga alichangia kutemwa kwa Bw Wetang’ula, mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa na Seneta wa Kakamega Cleophas Malala kama kiongozi wa wachache na kiranja wa wachache bunge la kitaifa na seneti mtawalia.

Hata hivyo, viongozi wa jamii ya ‘Mulembe’ hawastahili kumlaumu Bw Odinga kwa sababu ni siasa za waziri huyo mkuu wa zamani ndizo zimekuwa zikisababisha wakazi wa Magharibi kumuunga mkono.

Mwanzo, Bw Mudavadi amefaulu nyakati zote ambapo ameshirikiana na Bw Odinga kisiasa kinyume na alipoamua mkondo wake kisiasa.

Baada ya kuanguka kura vibaya mnamo 2002, ni Bw Odinga alimkweza Bw Mudavadi na kumfanya mgombeaji mwenza wake kisha akawa naibu waziri mkuu katika serikali ya muungano na pia waziri wa serikali za mitaa.

Katika serikali hiyo hiyo ya muungano, Bw Odinga aliwapa Wycliffe Oparanya, Ababu Namwamba, Fred Gumo, Paul Otuoma wizara mbalimbali, akawateua wanasiasa wengine kama mawaziri wasaidizi.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Suluhisho la kudumu dhidi ya baa la njaa...

Watu 4 wafariki katika ajali ya ndege ya mizigo ya Urusi

T L