Celtic na Midtjylland nguvu sawa kwenye mchujo wa UEFA

Celtic na Midtjylland nguvu sawa kwenye mchujo wa UEFA

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

KOCHA Ange Postecoglou alianza kazi kambini mwa Celtic kwa kuongoza waajiri wake kusajili sare ya 1-1 dhidi ya Midtjylland kwenye gozi la kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2021-22.

Timu zote mbili zilikamilisha mchuano huo na wachezaji 10 uwanjani baada ya Nir Bitton wa Celtic na Andres Dreyer wa Midtjylland kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika za 44 na 56 mtawalia.Liel Abada aliwaweka wenyeji Celtic kifua mbele katika dakika ya 39 kabla ya Da Silva Ferreira kusawazisha mambo katika dakika ya 66.

Mechi ya marudiano kati ya vikosi hivyo imeratibiwa kusakatwa mnamo Jumatano ijayo jijini Copenhagen, Denmark ambapo mshindi atasonga mbele kumenyana na PSV Eindhoven au Galatasaray katika raundi ya tatu ya mchujo.

Mechi ya Jumanne usiku iliyohudhuriwa na mashabiki 9,000 ilikuwa ya kwanza kwa kocha Postecoglou kusimamia mbele ya mashabiki baada ya kipindi cha wiki 16.

Celtic wanawania fursa ya kunogesha kampeni za UEFA kwa mara ya kwanza tangu 2017-18. Baada ya kurudiana na Midtjylland mnamo Julai 28, Celtic wameratibiwa kuanza kampeni zao za msimu wa 2021-22 kwenye Ligi Kuu ya Scotland mnamo Julai 31 dhidi ya Hearts ugenini.

 

  • Tags

You can share this post!

Everton wasajili fowadi Andros Townsend na kipa Asmir...

Arsenal wajiondoa kwenye Florida Cup baada ya kikosi...