Michezo

Celtic watiwa katika kundi moja na AC Milan kwenye Europa League

October 3rd, 2020 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

MABINGWA wa Kombe la FA, Arsenal, wametiwa kwenye Kundi B pamoja na Dundalk ya Ireland, Rapid Vienna na Molde katika kipute cha Europa League msimu huu wa 2020-21.

Tottenham Hotspur wamepangwa pamoja na mabingwa wa Bulgaria, Ludogorets, LASK na Royal Antwerp ya Ubelgiji kwenye Kundi J.

Leicester City watavaana na Braga, AEK Athens na Zorya Luhansk ya Ukraine kwenye Kundi G.

Mabingwa wa Scotland, Celtic watakuwa na kibarua kigumu kwenye Kundi H ambalo linajumuisha AC Milan, Lille na Sparta Prague.

Rangers wametiwa kwenye Kundi D kwa pamoja na Benfica, Standard Liege na Lech Poznan.

DROO YA EUROPA LEAGUE:

KUNDI A: Roma, Young Boys, Cluj, CSKA Sofia

KUNDI B: Arsenal, Rapid Vienna, Molde, Dundalk

KUNDI C: Bayer Leverkusen, Slavia Prague, Hapoel Beer-Sheva, Nice

KUNDI D: Benfica, Standard Liege, Rangers, Lech Poznan

KUNDI E: PSV Eindhoven, PAOK, Granada, Omonoia

KUNDI F: Napoli, Real Sociedad, AZ Alkmaar, Rijeka

KUNDI G: Braga, Leicester, AEK Athens, Zorya Luhansk

KUNDI H: Celtic, Sparta Prague, AC Milan, Lille

KUNDI I: Villarreal, Qarabag, Maccabi Tel-Aviv, Sivasspor

KUNDI J: Tottenham, Ludogorets, LASK, Royal Antwerp

KUNDI K: CSKA Moscow, Dinamo Zagreb, Feyenoord, Wolfsberger

KUNDI L: Gent, Red Star, Hoffenheim, Slovan Liberec