Chager afungua mwanya wa alama saba baada ya kushinda KCB Nakuru Rally

Chager afungua mwanya wa alama saba baada ya kushinda KCB Nakuru Rally

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa kitaifa wa mbio za magari za Kenya, Baldev Chager amechukua uongozi wa mapema wa msimu wa 2021.

Chager, ambaye hakuwa na ushindi katika duru ya Nakuru baada ya kuridhika na nafasi ya pili mwaka 2014 na 2018 na nambari tatu mwaka 2019, alinyakua ubingwa wa KCB Nakuru Rally katika ranchi ya Soysambu mnamo Februari 20.

Anaongoza jedwali kwa alama 33 baada ya kutawala katika maeneo ya Soysambu ambayo ni mojawapo ya sehemu zitakazotumiwa kwa mbio za dunia za Safari Rally mwezi Juni. Akielekezwa na Ravi Soni katika gari la Mitsubishi Evolution 10, alishinda mikondo mitano ukiwemo wa ‘power stage’ wa kupata alama tatu za bonasi kati ya saba ya Soysambu, akiibuka mshindi.

Chager alikuwa pia amepata kionjo cha sehemu nyingine mbio za Safari Rally zitafanyika aliposhiriki mashindano ya KCB Autocross mnamo Februari 14 katika shamba la Kasarani jijini Nairobi.

Dereva huyo anafuatwa katika jedwali la alama na madereva wenzake kutoka timu ya Kabras Sugar Racing Tejveer na Onkar Rai ambao wana alama 25 na 23, mtawalia.

Katika mahojiano, Chager alisema, “Ni heshima kubwa timu ya Kabras Sugar kufagia nafasi tatu za kwanza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10.”

Safari Rally itaandaliwa Juni 24-27 katika kaunti za Nairobi na Nakuru.

Onkar Rai, ambaye alikuwa amenyakua mataji na Nakuru mwaka 2017, 2018 na 2019, anafuatwa kwa karibu na jagina Ian Duncan ambaye amezoa alama 19.

Klabu ya la Kenya Motor Sport Club itaandaa duru ya pili katika kaunti ya Machakos mnamo Machi 27-28.

Msimamo wa Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) baada ya KCB Nakuru Rally:

Madereva

1 Baldev Chager alama 33

2 Tejveer Rai 25

3 Onkar Rai 23

4 Ian Duncan 19

5 Eric Bengi 17

6 Paras Pandya 15

7 Nikhil Sachania 13

8 Jasmeet Chana 11

9 Ghalib Hajee 9

10 Evans Kavisi 7

11 Daren Miranda 5

12 Edward Maina 4

13 Rajiv Ruparelia 3

Waelekezi

1 Ravi Soni alama 33

2 Gareth Dawe 25

3 Drew Sturrock 23

4 Anthony Nielsen 19

5 Peter Mutuma 17

6 Falgun Bhojak 15

7 Deep Patel 13

8 Ravi Chana 11

9 Sinder Suddle 9

10 Absolom Aswani 7

11 Wayne Fernandes 5

12 John Ngugi 4

13 Enoch Olinga 3

You can share this post!

Kocha Flick ahimiza Bayern Munich watumie mechi ya leo ya...

Raila akausha marafiki