Chebukati ahimizwa akaze mkono ili kumaliza taharuki

Chebukati ahimizwa akaze mkono ili kumaliza taharuki

NA TITUS OMINDE

WANACHAMA wa Bunge la Mwananchi na viongozi wa kidini kutoka Uasin Gishu wanaitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iharakishe kujumlisha na kuhakiki kura za urais, ili kuondoa hofu ambayo inaendelea kutanda.

Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kenya (CIPK) Sheikh Abubakar Bini anamtaka mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati kuharakisha shughuli ya kutangaza matokeo rasmi ili kuwawezesha Wakenya kumjua rais wao na kuendelea na shughuli nyingine.

Akirejelea hatua ya serikali kuahirisha kufunguliwa kwa shule, Sheikh Bin alisema tangazo la serikali la kuahirisha kufunguliwa kwa shule limewafanya wazazi wengi kuanza kudhani hali si shwari nchini.

“Siasa hazifai kukomesha shughuli muhimu nchini, Bw Chebukati sharti aharakishe matangazo ili wazazi wajue watoto wao wanaporejea shuleni,” alisema Sheikh Bin.

Sheikh Bin anataka IEBC itangaze matokeo ya hivi punde ifikapo Jumapili alasiri.

Maoni sawa yalitolewa na Angeline Anyango mfanyabiashara wa samaki katika mji wa Eldoret ambaye alisema wazazi wengi wana wasiwasi kutokana na kucheleweshwa kwa kutangaza matokeo huku akisisitiza kuwa, hatawaruhusu watoto kwenda shuleni hadi tangazo kuu litolewe.

“Wasiwasi wangu ni kwamba, tangu tulipopiga kura hatujaambiwa matokeo na tulikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa watoto wetu ikiwa shule zitafunguliwa kabla ya IEBC kutangaza matokeo,” alisema Bi Anyango. Hali ni vivyo hivyo Bunge la Mwananchi pale Telcom House.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: IEBC iweke kanuni nzuri za kuwachuja wasimamizi

Mvurya awazidi maarifa Joho na Kingi, Achani akichukua Kwale

T L