Chebukati asimulia mahangaiko yake, maafisa wa IEBC

Chebukati asimulia mahangaiko yake, maafisa wa IEBC

WINNIE ONYANDO

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati jana alisimulia kwa uchungu kile alichosema ni kuhangaishwa yeye mwenyewe, makamishna na wafanyikazi wa tume hiyo.

Bw Chebukati alisema kuwa hapo jana Jumatatu makamishna wawili, Bolu Moya na Profesa Abdi Guliye pamoja na afisa mkuu wa IEBC Marjan Hussein, walijeruhiwa viongozi wa Azimio walipowavamia katika jukwaa la kutangazia matokeo ya urais.

Bw Chebukati alieleza kuwa baadhi ya maafisa wa IEBC walikamatwa kiholela hata katika ukumbi wa Bomas, mmoja hajulikani aliko na wengine wamepewa vitisho.

Katika tukio la Jumatatu ambapo maafisa wa IEBC walijeruhiwa, vurugu zilianza baada ya maajenti wa Kinara wa ODM, Raila Odinga kuanza kuzozana punde tu Bw Chebukati alipofika katika ukumbi huo kutangaza matokeo.

Maajenti hao walidai kuwa Bw Chebukati alitoweka kwa muda kabla ya kuwapa fomu za matokeo ili wakague na walipomwona katika ukumbi huo wa Bomas walianza kumuandama wakimtaka awaonyeshe fomu hizo.

Vurugu zilizuka seneta mteule wa Narok, Ledama Ole Kina, gavana mteule wa Siaya, James Orengo na maajenti wengine wa Bw Odinga walipomshambulia Bw Chebukati, makamisha na maafisa wa IEBC.

Vurugu hizo zilifanya matangazo ya uchaguzi kucheleweshwa hadi saa kumi na mbili jioni kinyume na alivyotangaza awali Bw Chebukati.

Awali matangazo yalitarajiwa kutolewa saa tisa lakini yakawa yanaahirishwa.

  • Tags

You can share this post!

Achani afokea wanaompinga ugavana Kwale

Ruto abwaga Raila kuwa rais wa tano wa Kenya

T L