Chebukati awasihi Wakenya kuombea maafisa wa IEBC

Chebukati awasihi Wakenya kuombea maafisa wa IEBC

NA LEONARD ONYANGO

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amewataka Wakenya kumuombea huku akifichua kwamba yeye na makamishna wenzake wanapitia kipindi kigumu.

Bw Chebukati, aliyekuwa akizungumza wakati wa mkutano wa maombi na viongozi wa kidini katika Ukumbi wa Bomas jijini Nairobi mnamo Jumatano, ambapo ndipo kituo cha kitaifa cha kujumulisha matokeo ya urais kitakuwa, alisema familia za makamishna na maafisa wengine wa IEBC zinaishi kwa hofu.

“Familia zetu ndizo zinaumia zaidi kimyakimya. Hamuwezi kujua lakini wanandoa wetu na watoto wetu wanahitaji maombi ili wawe na ustahimilivu,” akasema Bw Chebukati.

“Ombeeni maafisa wa IEBC watakaosimamia uchaguzi katika maeneobunge yote 290 wakiwemo maafisa wa polisi ambao wanatupa ulinzi,” akasema.

Kulingana na Bw Chebukati, maafisa wa polisi wanaendelea na shughuli ya kusafirisha vifaa vya kura katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Bw Chebukati alitoa wito huo siku chache baada ya mkewe Mary, kufichua jinsi uchaguzi wa 2017 ulivyosababisha familia yake kuhangaika.

Bi Chebukati, aliyekuwa akizungumza Jumamosi, aliwataka Wakenya kumuombea mumewe ili kuweza kuongoza shughuli hiyo kwa njia ya amani na utulivu.

You can share this post!

Jinsi Wajackoyah alivyojimaliza kisiasa ghafla

Haki Africa yazindua kituo cha kufuatilia uchaguzi

T L