Chelsea na Fulham watoshana nguvu kwa sare tasa katika mechi ya EPL ugani Stamford Bridge

Chelsea na Fulham watoshana nguvu kwa sare tasa katika mechi ya EPL ugani Stamford Bridge

Na MASHIRIKA

LICHA ya kumchezesha Enzo Fernandez aliyevunja rekodi ya uhamisho wa wachezaji nchini Uingereza, Chelsea walikosa kuangusha Fulham waliowalazimishia sare tasa katika mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Ijumaa usiku ugani Stamford Bridge.

Wakipania kushinda mechi ya pili mwaka huu, Chelsea walimwajibisha Enzo hadi mwisho wa kipindi cha pili katika pambano hilo lililokuwa lake la kwanza ndani ya jezi za kikosi hicho cha kocha Graham Potter.

Fernandez ambaye ni raia wa Argentina, alitua Chelsea kwa Sh16.3 bilioni mnamo Januari 2023 baada ya kuagana na Benfica ya Ureno. Alianza mechi kwa matao ya juu na nusura afunge bao katika kipindi cha pili.

Kai Havertz, Hakim Ziyech na sajili mpya David Datro Fofana nao walipoteza nafasi za wazi za kufungia Chelsea mabao katika kipindi cha pili. Mykhailo Mudryk, Benoit Badiashile na Noni Madueke ndio wachezaji wengine wapya waliowajibishwa na Chelsea katika pambano hilo.

Matokeo ya mechi hiyo yaliacha Chelsea katika nafasi ya tisa kwa alama 30 sawa na Brentford ambao wana mchuano mmoja wa akiba. Fulham kwa upande wao walipaa hadi nafasi ya sita kwa alama 32, saba nyuma ya Manchester United na Newcastle United.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

STAA WA SPOTI: Huyu fowadi Felix Ojow ni moto otea mbali...

Ruto ateua Mwathethe kusimamia KEFRI

T L