Michezo

Chelsea yatuma Moses kambini mwa Spartak Moscow kwa mkopo

October 19th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

KIUNGO mvamizi wa Chelsea, Victor Moses ameingia katika sajili rasmi ya Spartak Moscow ya Urusi kwa mkopo wa kipindi cha mwaka mmoja.

Spartak watakuwa radhi kumpokeza sogora huyo raia wa Nigeria mkataba wa kudumu mwishoni mwa kipindi hicho cha mkopo.

Moses, 29, alichezea Fenerbahce ya Uturuki na Inter Milan ya Italia kwa mkopo msimu uliopita wa 2019-20.

Tangu ajiunge na Chelsea mnamo 2012, hakuna msimu hata mmoja ambao umeshuhudia Moses akihudumu ugani Stamford Bridge kwa zaidi ya miaka miwili.

Huu ni msimu wake wa sita akitumwa kwa mkopo na Chelsea ambao kwa sasa wanatiwa makali na kocha Frank Lampard.