China yatoa mchango muhimu kupunguza umaskini duniani

China yatoa mchango muhimu kupunguza umaskini duniani

NA MASHIRIKA

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umaskini, ambao umekumbusha mchakato wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC kilivyoongoza wananchi wa China kupambana na umaskini.

Waraka huo umesema China ikiwa nchi yenye idadi ya watu inayochukua karibu moja ya tano ya idadi ya watu wote duniani, mafanikio yake ya kutokomeza umaskini yametoa mchango mkubwa kwa ajili ya kazi ya kupunguza umaskini duniani na maendeleo ya binadamu.

Waraka huo umeonesha kuwa, tangu sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ianze kutekelezwa, kwa mujibu wa vipimo vya umaskini kwa hivi sasa, watu milioni 770 wenye matatizo ya kiuchumi vijijini kote nchini China wameondokana na umaskini, na kutokana na vipimo vya umaskini vya kimataifa vya Benki ya Dunia.

Idadi hiyo imechukua zaidi ya asilimia 70 ya ile ya dunia, hali inayoonesha kuwa China imetimiza lengo la kupunguza umaskini lililowekwa katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa miaka kumi mapema kabla ilivyopangwa.

Waziri wa mambo ya kilimo na vijiji Bw. Tang Renjian ameeleza kuwa, mafanikio ya kuondokana na umaskini ya China ni ya pande zote na ya kihistoria. Anasema:“Hadi sasa watu milioni 98.99 wenye matatizo ya kiuchumi, pamoja na wilaya 832 na vijiji laki 1.28 maskini vyote vimeondokana na umaskini, huku kiwango cha maisha ya watu kikiboreshwa kwa kiasi kikubwa.”

Waraka huo pia umefahamisha mpango wa China kuanzisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa. Naibu waziri wa Idara ya matangazo ya Kamati Kuu ya CPC Bw. Xu Lin anasema:“China imekuwa ikishiriki katika ushirikiano wa kimataifa wa kupunguza umaskini.”

“China imetoa mchango mkubwa kwa ajili ya kupunguza umaskini duniani na kuhimiza binadamu kupata maendeleo ya pamoja kwa kutokomeza kwa pande zote umaskini kabla ya muda uliopangwa katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.

“Pia inapenda kuimarisha ushirikiano huo, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kujenga Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ambayo haina umaskini na kupata maendeleo kwa pamoja.”

Bw. Xu pia amesisitiza kuwa, China bado ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, pia ina safari ndefu kabla ya kutatua suala la kutokuwa na uwiano kimaendeleo, kupunguza pengo la maendeleo kati ya vijiji na miji, na kutimiza maendeleo ya pande zote ya binadamu na utajiri wa pamoja wa watu wote.

CRI

  • Tags

You can share this post!

Umuhimu wa usawa wa kijinsia kielimu katika kupunguza...

KINA CHA FIKRA: Profesa Ken Walibora alikichapukia...