Chipukizi hodari wa chesi apania kuvunja rekodi mashindano ya Afrika

Chipukizi hodari wa chesi apania kuvunja rekodi mashindano ya Afrika

NA RUTH AREGE 

CHIPUKIZI wa mchezo wa chesi Christian Mwamba anajiandaa kwa mashindano ya Afrika ya Chesi yatakayofanyika Monrovia, nchini Liberia mnamo Disemba 2022.

Alishinda tiketi ya kuwakilisha Kenya baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya kitaifa yaliofanyika mjini Eldoret mwaka huu. Alikuwa nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi 272 walioshiriki. Mashindano ya Liberia yatahusisha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 10 na 11.

Mwanaspoti huyo mwenye umri wa miaka 10, alipoanza kucheza chesi kwenye mashindano tofauti anasema yalikuwa magumu. Alikufa moyo wakati mwingi na kuwa na wazo la kuacha kucheza.

“Mjomba wangu alianza kunifunza kucheza nikiwa na umri mdogo sana. Mnamo Novemba 2021 nilianza mashindano nikiwa na umri wa miaka tisa. Mashindano hayajakuwa rahisi, shindano la kwanza nilikuwa nafasi ya 22 lakini kadri muda ulivyosonga niliendelea kujiamini hadi nikafikia nafasi ya kwanza. Mashindano mjini Eldoret yalikuwa magumu sana lakini nilipambana. Nataka nikienda Liberia nirejee na medali, nina imani ninaweza,” akasema Mwamba.

Mamake Mwamba, Eva Wanjiku anasema, anajivunia mtoto wake ambaye anang’ara katika mchezo huo.

“Wakati huu mchache ambao tumekuwa tukimuelekeza, tumeona anauweza mkubwa wa kufanya vizuri katika mchezo huu akielekezwa vizuri. Tulitafuta kocha ambaye anamwelekeza kila siku. Tangia kuanza mchezo huu alitaka sana kushinda na kwa sasa yuko tayari kushindana,” alisema Wanjiku.

Kwa upande wa mwalimu mkuu wa Shule yake ya St. Marys Sportsview Academy Antony Kimani anakosomea Mwamba amemtakia kheri njema Mwamba wakati wa mashindano hayo.

“Katika shule yetu tunawapa wanafunzi hawa nafasi ya kucheza katika spoti tofauti tofauti. Mwamba anapeperusha bendera ya nchi yetu Juu zaidi na shule yetu piatunafuria. Atakapo enda Liberia tunamwombea ushindi,” aliongezea Kimani.

Kwenye mashindano mengine ambayo ameshiriki ya Chesi, Septemba 2022 alishinda Dhahabu kwenye mashindano ya Sanlam Invitation ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 10.

Mwezi huo huo, alishinda mashindano ya Shule za Kiafrika na pia mashindano ya Makini Open Youth Chess ambayo alinyakuwa dhahabu.

Kando na kucheza Chess pia anajihusisha na mchezo wa ‘Skating’ na ameshinda katika vitengo mbali mbali.

Alishinda Dhahabu na Fedha katika mashindano mbalimbali ya Mita 100 na Mita 1000 kuanzia mwaka 2019 hadi sasa.

Pia alishinda mashindano ya Kitaifa ya chini ya watoto wa miaka 10 ya utelezi mwaka 2022 na kushinda dhahabu.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge wamtaka Rais apunguze gharama

NGUVU ZA HOJA: Mabunge ya Kenya yatuzwa na chama cha...

T L