Chipukizi Jude Bellingham na Jamie Bynoe-Gittens wabeba Borussia Dortmund katika Bundesliga

Chipukizi Jude Bellingham na Jamie Bynoe-Gittens wabeba Borussia Dortmund katika Bundesliga

Na MASHIRIKA

CHIPUKIZI wa Uingereza, Jude Bellingham na Jamie Bynoe-Gittens walifunga bao kila mmoja na kusaidia Borussia Dortmund kutandika Augsburg 4-3 katika gozi la Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo Jumapili.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Bellingham kunogesha tangu taifa lake la Uingereza lidenguliwa na Ufaransa kwenye robo-fainali za Kombe la Dunia mnamo Disemba 10, 2022.

Augsburg walitoka nyuma kwa bao moja mara tatu hadi Dortmund walipofungiwa goli la ushindi na Giovanni Reyna katika dakika ya 78.

Bao jingine la Dortmund lilifumwa kimiani na Nico Schlotterbeck huku Augsburg wakipata magoli yao kupitia kwa David Colina, Arne Maier na Ermedin Demirovic levelled in stoppage time.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Sebastien Haller, 28, kuchezea Dortmund . Nyota huyo aliyejaza nafasi ya  Youssoufa Moukoko katika kipindi cha pili, alipatikana na ugonjwa wa saratani muda mfupi baada ya kuagana na Ajax ya Uholanzi na kutua Dortmund mnamo Julai 2022.

Ushindi wa Dortmund dhidi ya Augsburg uliwapaisha hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa jedwali la Bundesliga kwa alama 28, saba nyuma ya viongozi Bayern Munich.

MATOKEO YA BUNDESLIGA (Jumapili):

Borussia Dortmund 4-3 Augsburg

M’gladbach 2-3 Leverkusen

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Ushuru mpya wachemsha wauzaji wa miraa, muguka 001

Wasiwasi Urusi ikifanya ushauri na Afrika Kusini

T L