Michezo

Chipukizi wa Arsenal ataka kahaba arejee kwa ‘mechi ya marudiano’

August 4th, 2019 1 min read

NA MASHIRIKA

KIUNGO chipukizi wa Arsenal, Joe Willock, 19, sasa ametaka mwanamitindo Eglantine Flore Aguila kumpa fursa nyingine ya kulimenya tunda lake. Eglantine ambaye ni kahaba maarufu mzaliwa wa Ufaransa, amewahi pia kuwamegea tunda wanasoka Ashley Cole na Mario Balotelli.

Hadi alipomchezesha Willock miereka ya chumbani mwezi jana, Eglantine alikuwa akitoka kimapenzi na mwanamasumbwi Amir Khan, fowadi Saido Berahino wa Stoke City na aliyekuwa kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini.

Wiki jana, Willock alikiri kupagawishwa na weledi wa mchezo wa Eglantine chumbani na kubwa zaidi katika maazimio yake kwa sasa ni kumfanya kichuna huyo mwenye umri wa miaka 26 kuwa wake wa halali.

Willcok amewahi pia kujirinia asali mzingani mwa mwanadensi maarufu mzawa wa Australia, Dianne Buswell aliyetemana na mchumba wake Anthony Quinlan mwishoni mwa mwaka jana.

Awali, Eglantine alikuwa amepasua mbarika kuhusu uhusiano wake na Willock kupitia mtandao wa Instagram kwa kusisitiza kwamba kwa sasa penzi lake limepata hifadhi salama na ya kudumu moyoni mwa tineja huyo matata wa Arsenal japo ‘hakumfanyia kazi nzuri’ walipovaana kwa mara ya kwanza kimahaba.

Mnamo 2015, Eglantine alikiri kutoridhishwa na mchezo wa aliyekuwa beki wa Chelsea, Cole huku akitetea tukio la tunda lake kudokolewa pia na mvamizi wa sasa wa Olympique Marseille, Mario Balotelli.