Makala

CHOCHEO: Wajua waweza kufikia patamu kwa ndoto tu?

September 14th, 2019 2 min read

Na BENSON MATHEKA

SI lazima mtu ashiriki uroda ili aweze kujipata katika kilele cha tendo la ndoa.

Wataalamu wanasema mtu anaweza kupata raha peke yake bila kula uroda au kujichua.

Wanasema asilimia 80 ya wanaume na asilimia 40 ya wanawake hufikia kilele cha tendo la ndoa bila kula uroda.

Aidha wanasema mtu anaweza kupata ndoto zinazomfikisha kileleni maarufu kama ‘wet dreams’.

“Unaweza kupata ndoto hizi bila kuwa katika tendo la ndoa. Ni hali inayowapata baadhi ya watu,wanawake kwa wanaume,” asema mtaalamu wa masuala ya mahaba, Doris Yamben.

Vanessa Marin, mtaalamu mwingine wa masuala ya mapenzi anasema kuwa kufikia kilele cha tendo la ndoa ni suala la kisaikolojia linaloanzia katika akili ya mtu.

“Ingawa mtu hufikia kilele kwa kufanya mapenzi na mtu mwingine, ni hatua inayoanza akilini,” asema Vanessa.

“Si lazima mtu afanye mapenzi ili afike kileleni,” aongeza mtaalamu huyu.

Utafiti wa wanasayansi watajika wa masuala ya mapenzi Barry Komisaruk na Beverly Whipple, unaashiria kwamba wanawake wana uwezo wa kufikia kilele cha tendo la ndoa kwa kuzama kwenye mawazo yanayochochea hisia zao uroda.

Na katika utafiti mwingine, Komisaruk aligundua kuwa wanawake wanapofikiria kuhusu kupapasa matiti yao au sehemu nyingine za mwili zinazowasisimua, wanaweza kufika kilele cha tendo la ndoa peke yao hasa usiku.

“Nilichogundua kwa mshangao ni kuwa wakati wanawake wanapofikiria kuhusu mwili wao unaposisimka, wanaweza kuchangamka na kupandisha mzuka hadi kileleni,” aeleza Komisaruk katika utafiti uliochapishwa katika jarida la mtandaoni la Psychology Today.

Naye Jesse Kahn, asema kuwa ni habari njema hasa kwa watu ambao hawaridhiki wakati wa kula uroda kwa sababu ya mzongo wa mawazo, mfadhaiko na fedheha zinazochangiwa na desturi za kijamii.

“Kimsingi, usingizi ni mazingira mazuri ya kusababisha mtu kufika kilele cha tendo la ndoa,” anasema.

Uhuru

Kulala peke yako hukupa uhuru kuwazia mambo mengi ikiwa ni pamoja na mapenzi hivyo ni rahisi kuzamisha mawazo katika ngono.

“Haimaanishi kwamba mtu ana dosari fulani. Ni hali ya kawaida katika maisha ya binadamu. Kwa hakika, inaonyesha kwamba maisha yako ya mapenzi ni sawa,” aeleza Yamben na kuongeza kuwa hii haiwezi kuathiri afya ya mtu kama baadhi ya watu wanavyodhani.

“Kuna baadhi ya watu wanaopata ‘wet dream’ hizi mara kadhaa kwa wiki. Wengine huzipata mara chache katika maisha yao. Umri unavyozidi kuongezeka ndivyo ndoto hizi zinapungua,” aeleza.

Anasema hali hii sana sana huwapata watu ambao damu yao ingali moto.

Kulingana na wataalamu, sio lazima mtu aote akifanya mapenzi ili apate hali hii.

“Inaweza kutokea wakati wowote kwa watu ambao ni imara na wenye damu moto,” aeleza Joyce Kajuju, mtafiti wa masuala ya mapenzi wa shirika la Big Heart, Nairobi.

Anasisitiza kuwa hali hii huwa imejikita katika ubongo wa mtu na inaonyesha kwamba maisha yake ya tendo la ndoa ni imara.

Kuhusu ‘wet dreams’, wataalamu wanasema ni njia mojawapo ya kuondoa mihemko mwilini na sio kwamba mtu ana kasoro jinsi baadhi ya tamaduni zinavyoashiria.