Habari Mseto

Chumba cha wagonjwa mahututi Isiolo kuhamishwa

November 13th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mikakati imewekwa ili kuhamisha chumba cha wagonjwa mahututi waliougua corona kutoka chuo cha kufunza wamadaktari cha KMTC hadi jengo moja kwenye hospitali ya rufaa ya Isiolo.

Hii inatarajiwa kutoa nafasi kwa wanafunzi ili masomo irejee kama kawaida.

Gavana wa Kaunti ya Isiolo Mohamed Kuti alisema kwamba  mashinie za ICU ambazo zina thamani ya milioni moja zinatolewa chuoni humo wiki hii akiongeza kwamba  marekebisho yanaendelea kufanywa  ili kuhakikisha kwamba huduma bora zinatolewa.