Habari Mseto

CORONA: Kimya makanisani, waumini wakimbilia YouTube

March 29th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

TOFAUTI na Jumapili iliyopita ambapo makanisa mengine yalikaidi amri ya serikali ya kufunga makanisa maeneo ya mikusanyiko, Jumapili hii mambo yalikuwa tofauti.

Kulikuwa na kimya kingi katika makanisa mengi katika mitaa ya Nairobi huku milango ikisalia kufungwa.

Mabawabu pekee ndio walioonekana kuchunga makanisa huku hali halisi yaiwa virusi vya corona ikijitokeza kwa waumini ambao raundi hii walitumia simu zao kutazama ibada kupitia video za moja kwa moja kwenye YouTube.

Misikiti pia haikuachwa nyuma huku ikisalia kufungwa baada ya sala ya lazima ya asubuhi na mapema kusimamishwa.

Nyimbo za kumsifu na kumwabudu Mungu ambazo husikika kila Jumapili kutoka kwa makanisa mengi hazikusikika, ila waumia wengimitaani walifungulia kwa sauti ya juu ibada za redioni na kwa runinga.