Habari Mseto

CORONA: Mahakama ya Milimani yasalia mahame

March 27th, 2020 2 min read

NA RICHARD MUNGUTI

Mahakama kuu ya Milimani imesalia kuwa mahame kufuatia agizo la Jaji Mkuu David Maraga korti kote nchini zifungwe na wafanyazi wake wahudunu kutoka nyumbani.

Kwa sasa, ni maafisa wa polisi wa utawala wanaolinda majengo ya serikali pamoja na walinzi wa kampuni ys Gyto.

Mahakama hana watu hata! Hofu ya wa ugonjwa wa corona imeathiri huduma za mahakama. Picha/ Richard Munguti

“Hakuna mtu anaruhusiwa kuingia ndani. Wanaotaka kuhudumiwa watawasilisha hati zao kwa njia ya mtandao kwa idara husika,” mlinzi wa Gyto aliambia Taifa Leo Dijitali.

Afisa huyo alisema ikiwa wakili ama mshukiwa yuko na jambo la kuhudumiwa anawasiliana na idara husika kwa kuwasilisha ujumbe kwa baruapepe.

Afisa wa ulinzi wa mahakama akiweka arifa katika lango kuu la mahakama kuu ya Milimani, Nairobi. Picha/ Rcihard Munguti

“Ikiwa mtu analipia huduma anatumia nambari ya Mpesa iliyowekwa katika arifa iliyowekwa katika lango kuu,” afisa wa ulinzi aliyeajiriwa na idara ya mahakama Bw Mutune alidpkeza huku akiweka ujumbe kuhusu malipo.

Mwanakandarasi aliyejenga jengo lililoporomoka na kusababisha vifo vya watu sita alizuiliwa Jumatano kuingia katika mahakama ya Millimani kuhoji kuhusu kusikizwa kwa kesi hiyo.

Mwanakandarasi Jared Kabii akisoma arifa katika lango la Mahakama ya Milimani. Picha/ Richard Munguti

“Nilifika hapa mahakamani nikiwa tayari na kuebdelea na kesi lakini nimekuta mahakama imefungwa,” Bw Jared Kabii alisema.

Mjenzi huyo alikuwa ameagizwa na hakimu mkuu Francis Andayi afike kortini kesi inayomkabili ianze kusikizwa.

Lakini kesi hiyo haikuendelea kutokana agizo la Jaji mkuu David Maraga kwanba kesi zote sisuendelee.

Bw Kabii alizuiliwa kuingia katika afisi ya kushughulikia masuala ya umma.

 

“Nitajuaje lini kesi inayonikabili itakavyosikizwa?” Kabii aliuliza afisa wa ulinzi.

“Wasiliana na wakili wako atume ujumbe kwa njia ya mtandao kwa hakimu mkuu Francis Andayi,” alijibiwa.

Wakili David Ayuo akiwa nje ya mahakama ya Milimani baada ya kuzuiwa kuingia kujua hatma ya dhamana ya mteja wake. Picha/ Richard Munguti

Kesi dhidi ya Kabii ilikuwa imeorodheshwa kusikizwa mbele ya Bw Andayi Jumatano.

Huju akiendelea kuelezwa hayo Bw Andayi alitoka nje ya lango kusoma arifa iliyobandikwa nje ya lango.

Hakuzugumza na mtu. Aliisoma kisha akarudi ndani.

Wakili Ayuo azugumza na hakimu mkuu Francis Andayi ( kulia) kupitia kwa ua. Picha/ Richard Munguti

Maagizo ya Jaji mkuu David Maraga kuhusu malipo ya dhamana na pia faini yamezua mtafaruku.

Mawakili waliofika mahakamani kuhoji juu ya kesi zao Jumatano hawakupata majibu.

“Maagizo malipo yafanywe kupiitia kwa njia ya kielektronik yanakanganya;” alisema wakili Ayuo.

Wakili huyo hakuweza kujua uamuzi wa kupunguzwa kwa dhamana ya mteja wake ambaye amekuwa rumande tangu 2015.

Hakimu mkuu mahakama ya Milimani Francis Andayi (kushoto) akisoma arifa ya Jaji Mkuu David Maraga iliyobabandikwa katika lamgo la Mahakama kuu ya Milimani kuhusu malipo ya faini na ada za mawasilisho ya kesi. Picha/ Richard Munguti

” Mteja wangu anayekabiliwa na shtaka la ughushi wa stakabadhi alipunguziwa dhamana na mahakama kuu lakini sijajua kiwango kwa vile hakuna makarani katika idara ya usajili wanaoweza kuisoma faili na kunieleza ndipo niandae malipo,” Ayuo..

Pia hakuna afisa wa kutia sahini dhamana nikilipa dhamana ndipo mshtakiwa atoke gerezani.

“Natoa wito kwa Jajii Maraga aamuru kuwe na afisa wa kupokea nakala na pia kutia sahini hati za dhamaba,” Ayuo..

Wakili huyo alisena haki za washukiwa zimekandamizwa kabisa kwa vile hakuna kesi inayoendelea licha ya kuwa ba teknolojia ya kufanya kwa njia ya mtandao wa video.