Kimataifa

Corona sasa yasababisha uhaba wa shashi madukani

March 3rd, 2020 2 min read

MASHIRIKA Na MARY WANGARI

YAMKINI hii ndiyo maana hasa ya habari zinazotamba – heshitegi #karatasishashi imekuwa ikivuma katika mtandao wa kijamii nchini Australia.

Wanunuzi bidhaa waliopigwa na butwaa wamekuwa wakichapisha picha mitandaoni ya rafu tupu katika duka za jumla ambapo karatasi shashi chungunzima zilikuwa zikipangwa hapo mbeleni.

Virusi vya corona na hofu ya kupatikana bila bidhaa hiyo muhimu ya nyumbani imesababisha ripoti za watu kununua karatasi shashi kutokana na taharuki, na katika hali hiyo, Twitter imekuwa na kipindi cha kuvunja mbavu.

Baadhi ya wateja walikabiliwa na hali ya ukavu.

“Ulimwengu umeingiwa na kichaa! Duka tatu za jumla – hakuna karatasi shashi! Nilichosikia mwisho ni kwamba virusi vya corona vinasababisha maradhi yanayofanana na mafua si kuendesha kwa kasi isiyodhibitika! Nilifanikiwa kupata pengine kifurushi kilichokuwa cha mwisho katika Brisbane yote! Huenda nikaiweka eBay!” aliandika Anne Stubbs.

Uhaba zaidi

“Hamna aibu Woolworths South Yarra Niliagizia bidhaa kupitia mtandaoni leo asubuhi nikaja kuzichukua saa mbili baadaye na nikaelezwa vifurushi vya karatasi shashi nilivyokuwa nimelipia vilikuwa vimeisha! Vifurushi 7 viliingia leo na vikauzwa vyote katika muda wa saa 3! Punguzeni idadi kwa kila mteja!! Hatuna #karatasishashi,” alifoka Paris Dean.

Lakini kulikuwa na hasira na kukereka.

“Nimeshindwa na la kusema. Eneo hili limeingiwa na wazima. Nini tunachopitia jameni? Taharuki ya kitaifa kuhusu karatasi shashi?” alishangaa Mike Carlton.

Wengine walihoji kwamba kiasi cha karatasi shashi kilichokuwa kikinunuliwa na baadhi ya watu kilikuwa kikubwa kupita kiasi kutumika kwa majuma machache tu.

“Wapumbavu hawa kwani wanatarajia kwenda haja kubwa kiasi gani,” alifoka MaryTraine.

Wengine walielezea mawazo yao.

“Ninakisia kwamba kulingana na hali ilivyo katika duka nyingi, Ikiwa utapata virusi vya korona unakabiliwa na hatari ya kwenda haja hadi ufe,” alieleza Bi Woog.

Soko la magendo lilionekana kunoga.

Nina kifurushi cha 9 ambacho nitauzia mnunuzi atakayetoa bei ya juu zaidi. Ni laini mno. Ninahitaji kodi ya nyuma hivyo uanze kwa kutaja bei ya juu kabisa,” alisema Peter.

Wakati uo huo, baadhi walihoji kwamba hauhitaji karatasi shashi kuji…naam, kujisafisha vyema.