CORONA: Serikali yathibitisha visa vingine 9

CORONA: Serikali yathibitisha visa vingine 9

NA FAUSTINE NGILA 

WATU wengine tisa wamepatikana na virusi vya corona Jumanne na kuongeza idadi ya walio na virusi hivyo kutoka 50 hadi 59.

Akihutubia taifa Jumanne, Naibu Waziri wa Afya Dkt Mercy Mwangangi alisema kuwa watu 234 walipimwa na kati yao tisa wakapatikana kuwa na virusi hivyo.

Alisema kuwa maafisa wanaendelea kutafuta watu wanaoweza kuwa walitangamana na wagonjwa hao.

Dkt Mwangangi alitangaza kuwa shule za bweni zitatumika kama vituo vya kutenga wagojwa kwa  hospitali hazina nafasi ya kutosha.

Mpango huo utasaidia wakati wagojwa wataongezeka hospitalini ili kudhibiti visa vipya vya maambukizi.

“Tunachunguza utumizi wa shule za bweni ili kuongeza uwezo wetu iwapo visa hivi vitaongezeka zaidi”,Dkt Mwangagi alisema bila kutoa maelezo zaidi.

You can share this post!

Mgonjwa wa kwanza wa corona afariki Tanzania

Maseneta wenye zaidi ya miaka 58 kufanyia kazi nyumbani

adminleo