Habari

CORONA: Waislamu washauriwa kusali nyumbani

March 16th, 2020 2 min read

CECIL ODONGO na SAMUEL KAZUNGU

KADHI Mkuu Silicone, bodybuilding and samba: Bianca, carnival queen in Rio reveals her secrets cabergoline cabaser wrist power ball. Sheikh Ahmed Muhdhar amewashauri Waislamu watekeleze ibada zao nyumbani badala ya msikitini kama njia ya kutii agizo la serikali kuhusu mikusanyiko ya umma.

Bw Muhdhar alisema agizo la serikali kutaka watu wasijazane eneo moja ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona ni kwa manufaa ya Wakenya wote ndiyo maana Waislamu pia wanafaa kuchukua tahadhari na kulitii.

“Dua ya Waislamu hukubalika mahala popote ndio maana tunawaomba ikibidi watekeleze ibada zao nyumbani au waingie misikitini kwa makundi madogo nyakati tofauti,” akasema Sheikh Muhdhar.

Vilevile Sheik Muhdhar alitoa wito kwa Waislamu kufanya ibada kuhusu virusi hivyo ambavyo vimesitisha safari za baadhi yao kutembelea maeneo matakatifu jijini Makka, Saudi Arabia.

Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu (SUPKEM) Hassan Ole Naado naye aliwataka Waislamu wapunguza kupigana pambaja na salamu za mkononi huku pia wajinadhifisa mara kwa mara kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.

“Ningependa kuwashauri Waislamu wapunguze pambaja na salamu za mkononi japo ni itikadi ya dini yetu kujuliana hali kupitia njia hizo mbili. Ikizingatiwa kwamba sisi hushika ‘wudu’ kabla ya kuingia msikitini kuswaki ni vyema tufuate agizo la wizara ya afya tunapokuwa msikitini,” akasema Bw Ole Naado.

Katika Kaunti ya Lamu, baadhi ya viongozi wameapa kutoacha ada ya kusalimiana kwa mkono.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Muungano wa Viongozi wa kidini Pwani (CICC), Ustadh Mohamed Abdulkadir, masheikh na maimamu hao walishikilia kuwa hawaoni sababu ya waumini misikitini kukosa kujuliana hali kupitia salamu za mkono kwa sababu ya kuogopa virusi vya corona.

Bw Abdulkadir aliwahimiza waumini kuendelea kudumisha usafi wao kama ilivyo ada ya Muislamu huku akiitaka serikali kutafuta mbinu mwafaka za kukabiliana na ugonjwa huo.

Imamu wa Msikiti wa Markaz Habib Swaleh kisiwani Lamu, Said Khitamy alisema tayari wameanzisha kampeni kabambe misikitini, mitaani na mabarazani katika kuwaelimisha watu jinsi watakavyochukua tahadhari za mapema kuepuka kuambukizwa.