Corona: Watu 700,000 kufariki Ulaya katika miezi minne ijayo

Corona: Watu 700,000 kufariki Ulaya katika miezi minne ijayo

Na AFP

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa watu 700,000 huenda wakaaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19, unaosababishwa na virusi vya corona, kufikia Machi mwaka ujao.

WHO ilisema msimu wa baridi unaoshuhudiwa barani Ulaya, utasababisha ongezeko la vifo hivyo.Inakadiria kuwa idadi ya wanaofariki kwa Covid barani Ulaya itaongezeka kutoka milioni 1.5 sasa hadi milioni 2.2 kufikia Machi mosi.

Shirika hilo la afya pia linatarajia ongezeko la wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura katika nchi 49 kati ya 53 za Ulaya, kati ya sasa na Machi 2022.

Mataifa kadhaa ya Ulaya yameshuhudia ongezeko la wagonjwa wa Covid-19, wakati Austria ikiweka vikwazo vipya vya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo unaoshambulia mapafu.

Ujerumani na Uholanzi zinajitayarisha kutangaza vikwazo vipya vya kukabiliana na virusi vya corona.

You can share this post!

Raia mwingine wa kigeni apatikana amefariki ndani ya meli...

Malawi yamsihi Mike Tyson awe balozi wake wa bangi

F M