Corona yachangia wanafunzi 400,000 kukatiza masomo

Corona yachangia wanafunzi 400,000 kukatiza masomo

Na FAITH NYAMAI

ZAIDI ya wanafunzi 400,000 wa shule za msingi na upili walikatiza masomo yao kati ya Machi 2020 na Machi 2021 kutokana na athari za janga la Covid-19.

Mlipuko wa ugonjwa huo hatari ulichangia kufungwa kwa shule zote nchini kwa zaidi ya miezi saba.

Kulingana na ripoti kuhusu Hali ya Kiuchumi nchini mwaka wa 2021, idadi ya wanafunzi katika shule za msingi ilishuka hadi milioni 10 kufikia Machi 2021 kutoka milioni 10.2 mnamo Machi 2020 kutokana na athari za ugonjwa huo.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS) pia inaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 233,300 wa shule za upili hawakuripoti shuleni zilipofunguliwa Januari 2021.

Kwa ujumla idadi ya wanafunzi wa shule za msingi na upili waliokatiza masomo yao ni 433,300.

Ripoti hiyo inasema hali hiyo ilisababishwa na mimba, ndoa za mapema na changamoto nyingine za kijamii kama ajira ikizingatiwa kuwa shule zilifungwa kwa kipindi kirefu.

Data zinaonyesha mnamo Machi 2020, shule za msingi za umma zilikuwa na jumla ya wanafunzi 8,533,326.

You can share this post!

Chebukati aonya dhidi ya kampeni hizi za mapema

Laikipia yalipia makosa ya Wakoloni