Habari Mseto

Corona yamuua muuguzi Mombasa

October 26th, 2020 1 min read

NA WINNIE ATIENO NA FAUSTINE NGILA

Muuguzi mmoja katika Kaunti ya Mombasa alifariki kutokana na virusi vya corona Jumanne. Maafisa walisema kwamba afisa huyo alipata matatizo ya kupumua kabla ya kukimbizwa hospitali ya Likoni alipofariki.

Kufuatia kifo chake wezake walitengwa ilikuzia kusambaa kwa virusi hivyo..

Mwili wa muuguzi huyo utapelekwa nyumbani kwao Nyeri kwa mazishi. Muuguzi huyo alifanya kazi kwa miaka mingi kwenye hospitali ya Coast General kabla ya kuhamisha hadi hospitali ya Likoni.

“Tunasitikika kupoteza mmoja wetu  kwasababu ya virusi vya corona.Serikali ya kaunti imetutekeleza wakati huu wa janga la corona .Tuliomba serikali ya kaunti itupe vifaa vya kujikinga na virusi vya corona Pamoja na mshahara wetu wa mwezi Septemba lakini wamekaa kimya ,” ulisema mweyekiti wa muungano wa wauguzi Mombasa Peter Maroko.

Muungano wa maafisa hao wa afya ulisema kwamba walikuwa wanafanya kazi bila vifa vya kuwakinga kutokana na virusi vya corona.

Wauguzi hao wanataka wizara ya afya kuwashunulikia. Akizungumza na Taifa Leo Bw Maroko alisema kwamba kuanzia Ijumaa alipokea wauguzi watatu waliokuwa na virusi vya corona.

Alisema kwamba serikali haifanyi kazi yake.