Habari Mseto

Corona yamzuia Waititu kufika kortini

August 28th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Kesi ya aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu iliyokuwa iendelee  Jumatatu ilisitishwa baada  ya gavana huyo kukosa kufika kortini.

Hii ni baada ya wakili wake John Swaka kusema kwamba Bw Waititu alipatikana na virusi vya corona.

Korti ilisema awasilishe stakabathi za  hospitali wakati kesi hiyo itatajwa ili kuthibitisha kwa mkurugenzi wa  mashataka ya umma kuw aliugua virusi hivyo.