Habari Mseto

Corona yasitisha shughuli katika Bunge la Kaunti ya Mombasa

October 28th, 2020 1 min read

SIAGO CECE NAFAUSTINE NGILA

Bunge la Kaunti ya Mombasa limesitisha shughuli zake kwa muda wa wiki mbili baada ya madiwani watatu kupatikana na virusi vya corona.

Naibu Spika wa bunge hilo Fadhili Makarini alisema madiwani hao walipatikana wameambukiza corona baada ya vipimo kufanywa wiki iliyopita.

Vikao vya bunge vilikuwa virudi Jumanne baada ya likizo iliyowekwa ili kudhibiti msambao wa virusi vya corona.

“Tumesitisha vikao ili kupata nafasi ya kupima madiwani wengine,”aasliema Bw Makarani huku akiogeza kwamba madiwani hao walikuwa tayari wametengwa na wengine kuomba kujikarantini.

“Tutanyunyuzia dawa na tufuate maangizo mengine yaliyotolewa na wizara ya afya.Maafisa wote wanajua kwamba watapimwa.Kulingana na uwepo wa vifaa vya kupima mwishoni mwa wiki.”

Kusitishwa kwa vikao kutaleta madhara kubwa kwani kuna mishwada ambayo bado inagija kupitishwa huku zingine zikisubiri kupitishwa.