Habari

COVID-19: Kenya yathibitisha visa 23 vipya idadi jumla ikipanda hadi 672

May 10th, 2020 1 min read

Na MWANDISHI WETU

IDADI ya visa vya watu waliogundulika kuwa na maradhi ya Covid-19 nchini Kenya imepanda hadi 672 baada ya Wizara ya Afya kutangaza Jumapili visa 23 vipya.

Wagonjwa 22 ni Wakenya naye mmoja ni raia wa Burundi.

Kimaeneo, Mombasa imekuwa na wagonjwa 12 ikifuatwa na Mandera iliyo na wagonjwa sita nalo jiji kuu Nairobi likiwa na wanne ambao wametokea maeneo ya Umoja, Komarock, na Pipeline.

Nayo Kaunti ya Kajiado imekuwa na kisa kimoja.

Hii ni baada ya sampuli 1,056 kufanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya vipimo ambavyo vimefanywa nchini kufikia sasa ni 32,097.