Habari

COVID-19: Kenya yathibitisha visa 52 vipya

May 22nd, 2020 1 min read

Na MAGDALENE WANJA

WIZARA ya Afya imetangaza visa 52 vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Idadi jumla ya visa sasa ni 1,161 nchini Kenya.

Katika kikao cha kutoa taarifa za kila siku Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amewaambia wanahabari, mara hii akiwa Kaunti ya Machakos, kwamba kaunti za Nairobi na Mombasa ndizo zinaendelea kuandikisha idadi ya juu ya maambukizi.

Sampuli  2,567 zimefanyiwa vipimo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Katika visa hivyo vipya, Nairobi ina visa 23, Mombasa (7) na Busia (7).

“Ningetaka Kaunti ya Busia ichukue tahadhari zaidi kwani iko katika mpaka wa Kenya na Uganda ambao una idadi kubwa ya madereva wa matrela. Madereva hao wanahitajika kupimwa saa 48 kabla ya kusafiri,” amesema waziri Kagwe.