COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 280 idadi jumla ikifika 104,780

COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 280 idadi jumla ikifika 104,780

Na CHARLES WASONGA

KENYA imenakili visa 280 vipya vya maambukizi ya Covid-19 huku watu wawili zaidi wakifariki kutokana na ugonjwa huo.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Afya iliyotumwa Jumatano, visa hivyo vipya vimegunduliwa baada ya sampuli kutoka kwa watu 4,919 kupimwa ndani ya muda wa saa 24 zilizopita. Hii ina maana kuwa kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 5.6.

Visa hivyo vimefikisha idadi jumla ya maambukizi nchini Kenya kuwa 104,780 kutokana na idadi jumla ya vipimo 1,278,200 vilivyofanywa tangu kisa cha kwanza kilipogunduliwa mwaka jana.

Vile vile, vifo vya wagonjwa wawili sasa vimefikisha idadi jumla ya vifo kuwa 1,839.

Habari njema ni kwamba jumla ya wagonjwa 713 wa corona walithibitishwa kupona na hivyo kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa 86,378.

“Watu 676 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani ilhali 37 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini wakipokea matibabu,” ikasema taarifa hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Waziri Mutahi Kagwe.

Wizara hiyo imeongeza kuwa jumla ya wagonjwa 344 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini wakiugua Covid-19 ilhali wengine 1,495 wanahudumiwa nyumbani.

“Kati ya hao 55 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi huku wengine 22 wakisaidiwa kupumua kwa mitambo spesheli. Nao wagonjwa 22 wanaongezewa hewa ya oksijeni.

Visa vipya vilipatika katika kaunti zifuatazo: Kaunti ya Nairobi ilinakili visa 185, Nakuru (19) , Kiambu (19), Kericho (12), Mombasa (6), Kajiado (6), Murang’a (6), Uasin Gishu (6), Machakos (5), Meru (4) na Embu (3). Nazo kaunti za Bungoma, Busia, Garissa, Kirinyaga, Kisii, Kwale, Makueni, Nyandarua na Taita Taveta, ziliandikisha kisa kimoja kila moja.

You can share this post!

Wazazi washauriwa kuangazia majukumu yao

Mshtakiwa ageuzwa shahidi katika kesi ya ukwepaji ushuru