COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 335 idadi jumla ikifika 97,733

COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 335 idadi jumla ikifika 97,733

Na CHARLES WASONGA

WATU 335 zaidi wamethibitishwa Alhamisi kuwa na virusi vya corona nchini Kenya baada ya sampuli kutoka kwa watu 5,424 kupimwa ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita.

Kulingana na taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, wagonjwa wanane zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo ndani ya muda huo. Kwa hivyo idadi jumla ya wale waliofariki ni 1,702.

“Visa hivyo vipya sasa vinafikisha idadi jumla ya maambukizi ya Covid-19 nchini kufika 97,733 baada ya kupimwa kwa jumla ya sampuli 1,075, 673,” akasema Bw Kagwe.

Kulingana na taarifa hiyo, jumla ya wagonjwa 340 walithibitishwa kupona corona na kuruhusiwa kurejelea shughuli zao za kawaida. Hii ina maana kuwa kufikia Alhamisi jumla ya wagonjwa 80,306 wamepona corona.

Na 261 kati ya wale waliopona Alhamisi walikuwa wakiuguzwa nyumbani huku 79 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini wakipokea matibabu.

Visa vipya vya maambukizi vilivyonakiliwa nchini vimesambaa katika kaunti kama ifuatavyo; Nairobi inaongoza ikiwa na visa 102, Meru (46), Makueni (40), Nyeri (19), Kajiado (14) , Embu (13), Mombasa (12) na Kiambu (11),

Kaunti za Nakuru, Migori, Nyandarua na Busia kila moja zimeandikisha visa vipya tisa, Samburu (8), Kirinyaga (6) , Machakos (5) , Kitui (4), Turkana (4), Laikipia (3), Uasin Gishu (3), Siaya (3) na Kilifi visa viwili. Kaunti za Marsabit, Narok, Murang’a na Taita Taveta nazo zimenakili kisa kimoja kila moja.

You can share this post!

AKILIMALI: Aamini unyunyiziaji huu utaifanya Kenya kupiku...

KBF yawahakikishia Wakenya Preston Bungei atapeperusha...