Covid-19: Kisa cha kwanza Embu charipotiwa gerezani

Covid-19: Kisa cha kwanza Embu charipotiwa gerezani

NA MWANDISHI WETU

Huku janga la corona likiendelea kuenea kila siku, kisa cha kwanza gerezani kimeripotiwa.

Mahabusu mmoja katika Gereza la Embu alithibitishwa kuwa na virusi vya corona hapo Alhamisi, na kuandikisha kisa cha kwanza katika kaunti hiyo.

Mfungwa huyo ametengwa na atasafiriswa Nairobi kwa matibabu kulingana na Gavana wa Embu Martin Wambora.

Bw Wambora alisemamfungwa huyo anatoka Kaunti ya Tharaka Nithi na alikuwa ameletwa kwa gereza la Embu kwa makosa ya wizi.

“Ningependa kuthibitisha kwamba tunashungulikia kisa hicho cha kwanza  Embu lakini mwathiriwa anatoka Chuka,” alisema.

Maafisa wanashungulika kuchunguza kama mgonjwa huyo alitangamana na wengine.

You can share this post!

Mungiki wazimwe kabisa Mlima Kenya – Kibicho

Mawakili walaumu mahakama kwa kupanga kutupa maelfu ya kesi

adminleo