Habari Mseto

COVID-19: Mbunge wa Lunga Lunga ahimiza wakazi kuzingatia taratibu

December 6th, 2020 1 min read

Na WINNIE ATIENO

MBUNGE wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani amewaonya wakazi dhidi ya kupuuza maagizo ya kuzuia maambukizi ya corona.

Bw Mwashetani ambaye aliongea baada ya kuzika mkazi eneo la Kitungure, alisema anasikitishwa na idadi kubwa ya watu wanaoendelea kuaga dunia kufuatia janga hilo.

Alisema marehemu Kassim Zonzo alifariki ikiwa ni muda wa siku chache tu baada ya kuugua.

“Inashtusha kuona idadi kubwa ya watu wanaoaga dunia kila siku kufuatia janga hili. Kadhalika ninasikitishwa na namna ya wakazi wanavyopuuza maagizo ya kukabiliana na virusi hivi hasa vijijini,” alisema akionya hatari wakazi wanakodolea macho kwa kutozingatia maagizo.

Serikali ya kaunti ya Kwale imekuwa ikiwahimiza wakazi kufuatia maagizo ya afya ya umma imiwemo kuvaa barakoa, kuosha mikono na kutotangamana ndio wazingatie taratibu za kukabiliana na janga hilo. Hata hivyo wakazi wengi wamekuwa wakisusia maagizo hayo.