Michezo

COVID-19: Mkuu wa La Liga asisitizia wachezaji umuhimu wa kufuata maagizo

May 25th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

MADRID, Uhispania

MKUU wa Ligi Kuu ya La Liga, Javier Tebas ametoa onyo kali kwa wanasoka nchini hapa baada ya wawili wa klabu ya Sevilla kupuuza maagizo ya serikali kuhusiana na sheria za kutangamana.

Wanasoka Ever Banega, Lucas Ocampos na Franco Vazquez pamoja na mshambuliaji Luuk de Jong walionekana pichani mwishoni na watu wengine wanane kwenye karamu.

Tebas amesisitiza kwamba lazima wachezaji waonyeshe mfano mwema katika vita vya kupigana na ugonjwa wa corona.

“Wachezaji sharti wawe mfano bora kwa jamii na lazima wajiadhari kila wakati,” Tebas alisema kwenye hotuba yake kupitia kwa televisheni.

“Hata mazoezini lazima tujilinde kwa sababu maisha ya watu wengi yamo hatarini kwa sasa. Lazima tujiadhari,” aliongeza.

Uhispania ilikuwa imepiga marufuku watu kukutana baada ya taifa hili kurekodi visa kadhaa vya walioamnbukizwa maradhi ya COVID-19, mbali na mamia ya waliopoteza maisha yao kutokana na janga hilo.

Lakini majuzi ililegeza masharti yake baada ya visa hivyo kupunguka, ingawa haikubalii watu 10 kukutana.

Mbali na mkusanyiko wao, wachezaji nyingine iliwaonyesha wakimumunya kileo cha shisha.

Hatimaye, klabu ya Sevilla ilituma msamaha kwa niaba ya wachezaji hao, lakini hakusema iwapo wataadhibiwa.

Shughuli za michezo nchini hapa zilipigwa marufuku tangu Machi 12 kutokana na maambukizi ya COVID-19, lakini huenda zikarejelewa Juni 8.