Habari

COVID-19: Visa jumla nchini ni 12,062 waliofariki wakiwa wagonjwa 222

July 17th, 2020 2 min read

CHARLES WASONGA na SAMMY WAWERU

MTOTO mwenye umri wa miezi mitano ni miongoni mwa watu 389 zaidi ambao wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 katika kipindi cha saa 24 kufikia Ijumaa, Julai 17, 2022.

Sasa idadi jumla ya watu walioambukizwa ugonjwa huo tangu ulipolipuka kwa mara ya kwanza nchini imefika 12,062 baada ya jumla ya sampuli 233,641 kupimwa.

Akitoa taarifa kuhusu hali ya janga hilo nchini, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema wagonjwa hao 389 wapya walipatikana baada ya sampuli 3, 545 kupimwa ndani ya kipindi cha saa 24.

Miongoni mwao 260 ni wa jinsia ya kiume na 129 ni wa jinsia ya kike huku mwenye umri wa juu zaidi akiwa na umri wa miaka 95.

“Kwa bahati mbaya tumewapoteza wagonjwa watano kutokana na Covid-19, hivyo kufikisha 222 idadi ya vifo kufikia Ijumaa,” amesema Bw Kagwe akiwa katika Kaunti ya Muranga ambako amezuru kukagua vituo vya huduma za afya.

Kati ya wanne hao watatu walikuwa na magonjwa mengine kama kisukari na shinikizo la damu.

Bw Kagwe alizindua hospitali ya kimisheni ya Kiria-ini ambayo ina mitambo ya kisasa na ambayo itasaidia huduma kwa wagonjwa katika kaunti ya Muranga.

Waziri pia alikana madai kuwa maaraba ya kupima corona yamefungwa nchini, akisema hayo ni madai ya uwongo.

Wakati huo huo, Bw Kagwe amewahisi wanaume kuwaiga wanawake kwa kuwa na mazoea ya kuvalia barakoa kila wakati na kila mahali.

“Nafurahishwa zaidi na akina mama wetu kwa sababu ni watiifu zaidi kwa kanuni ya wizara yetu ya kuvalia barakoa. Lakini wanaume wetu wanalegea kidogo na nina wahimiza wawaige akina mama hawa,” amesema Bw Kagwe huku akikariri wito wa serikali kwamba ni wajibu wa raia kujikinga dhidi ya maambukizi ya Covid-19.

Akitoa takwimu hizo katika Hospitali ya Kimisheni ya Kiriaini, Mathioya Kaunti ya Murang’a ambapo ameendeleza ziara yake kukagua maandalizi ya kaunti mbalimbali katika kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona, Waziri amesema Nairobi inaendelea kuongoza katika maambukizi.

Kufikia Ijumaa, Nairobi imeandikisha jumla ya visa 6,751 tangu kisa cha kwanza cha Covid-19 kithibitishwe nchini mnamo Machi 13, 2020, Mombasa (1,784) na Kiambu (666).

Bw Kagwe ametangaza kwamba katika kipindi cha saa 24 zilizopita, wagonjwa watano wamefariki kutokana na corona, idadi hiyo ikifikisha jumla ya 222 walioangamizwa na Covid-19.

“Kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa huu, tuzidi kuzingatia sheria na mikakati iliyowekwa. Kwa watu wanaoishi mashambani, mjihadhari kutangamana na watu wanaotoka Nairobi na Mombasa, ikikumbukwa kuwa zuio la kuingia na kutoka nje ya kaunti hizo liliondolewa,” akasema.

Kufikia sasa, Kenya imefanya ukaguzi na vipimo jumla ya sampuli 233,641