Habari

COVID-19: Visa vingi zaidi vyaandikishwa

November 4th, 2020 1 min read

Na CHARLES WASONGA

KWA mara nyingine Kenya imeandikisha idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya virusi vya corona ndani ya saa 24 baada ya jumla ya watu 1,494 kugunduliwa kuwa na virusi hivyo.

Idadi hiyo iliyotangazwa Jumatano inazidi idadi ya visa vilivyothibitishwa Jumamosi, Oktoba 31, 2020, ambapo watu 1,395 waligunduliwa kuambukizwa virusi vya corona ndani ya saa 24.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema visa hivyo vipya vya maambukizi vilitokana na jumla ya sampuli 8,836 zilizopimwa ndani ya saa 24 na hivyo kufikisha 717,172 idadi jumla ya visa.

Wagonjwa 586 waliruhusiwa kuondoka kurejelea maisha yao ya kawaida baada ya kupona ambapo 413 kati yao walikuwa chini ya utunzaji wa nyumbani nao 173 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini.

Kwa hivyo, idadi jumla ya wagonjwa ambao wamepona kufikia Jumatano ni 39,381.

Kwa masikitiko, jumla ya wagonjwa 12 walifariki kutokana na Covid-19 na hivyo kufikisha 1,051 idadi jumla ya maafa kutokana na ugonjwa huo tangu mlipuko wake kutangazwa nchini Machi 13, 2020.

Wakati huu, jumla ya wagonjwa 1,313 wa corona wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku 5, 005 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 57 wako katika vyumba vya kuwahudumia wagonjwa mahututi (ICU), 25 wanahitaji usaidizi wa kupumua, 27 wanahitaji kuongezewa safi na 77 wako katika wadi za kawaida nyumbani ilhali 173 walikuwa amelazwa katika hospitali mbalimbali nchini.

Kwa hivyo, idadi jumla ya wagonjwa ambao wamepona kufikia Jumatano ni 39,381.

Kwa masikitiko, jumla ya wagonjwa 12 walifariki kutokana na Covid-19 na hivyo kufikisha 1,051 idadi jumla ya maafa kutokana na ugonjwa huo tangu mlipuko wake kutangazwa nchini Machi 13, 2020.

Wakati huu, jumla ya wagonjwa 1,313 wa corona wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku 5,005 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 57 wako katika vyumba vya kuwahudumia wagonjwa mahututi (ICU), 25 wanahitaji usaidizi wa kupumua, 27 wanahitaji kuongezewa safi na 77 wako katika wadi za kawaida.