UDAKU: CR7 amfunga Georgina hat-trick safi ya mapenzi

UDAKU: CR7 amfunga Georgina hat-trick safi ya mapenzi

Na CHRIS ADUNGO

SUPASTAA wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, na mchumba wake Georgina Rodriguez sasa wanatarajia watoto pacha watakaozaliwa mwakani.

Kwa mujibu wa jarida la Hola nchini Uhispania, Georgina ana ujauzito wa miezi mitatu na anatazamiwa kujifungua Aprili 2022.

Georgina amekuwa akitoka na Ronaldo, 36, kimapenzi tangu 2016. Ni mwanamitindo raia wa Uhispania.Ronaldo, maarufu kama CR7, tayari ni baba wa watoto wanne.

Ujio wa watoto wawili zaidi utamweka karibu na ndoto yake ya kuwa na watoto saba; ili idadi hiyo iwiane na nambari ya jezi yake kambini mwa Man-United na timu ya taifa ya Ureno.

Georgina alijaliwa mtoto wa kike, Alana Martina, miaka mitatu iliyopita.Analea pia watoto wengine watatu wa Ronaldo – Cristianinho Jr pamoja na mapacha Eva Maria na Mateo Dos Santos.

Mateo na Maria walizaliwa na mwanamke raia wa Amerika mnamo Juni 2017, baada ya Ronaldo kutoa mbegu zake za kiume zilizokutanishwa na yai la kichuna mmoja mzawa wa Uhispania, ambaye alimlipa Sh2.8 bilioni.

Mwanamke aliyejitolea kubeba mimba hiyo mwishoni mwa Septemba 2016 alipokezwa kima cha Sh1.5 bilioni.

Ronaldo aliwahi pia kutumia kima cha Sh1.2 bilioni kulipia yai la mwanamke raia wa Mexico mnamo 2010.

Baada ya yai hilo kukutanishwa na mbegu zake, Ronaldo alimpa mwanamke mwingine mwenye asili ya Mexico kima cha Sh1.4 bilioni, kubeba ujauzito ambao uliishia kuzaliwa kwa mwanambee wake Cristianinho Jr, 11.

Akitumia mitandao yake ya kijamii, Ronaldo alipakia picha aliyopigwa pamoja na Georgina wakishikilia picha ya matokeo ya uchunguzi wa ujauzito wa kipusa huyo, aliyewahi kuwa yaya na mhudumu wa dukani.

“Furaha isiyo kifani kwamba tunatarajia mapacha. Mioyo yetu imejaa mapenzi na tunasubiri kwa hamu kubwa kukutana nanyi,” akaandika Ronaldo.

Naye Georgina pia alisema: “Hamu yangu ya kuwa mama kwa mara nyingine ni kubwa kuliko kitu chochote kingine. Sitakomea kwa hawa wawili ninaotarajia. Nina kiu ya kujaza dunia.”

Mwanzoni mwaka huu, Georgina alisema yuko tayari kumzalia Ronaldo watoto watatu zaidi ila kwa masharti.

Mbali na kumtaka sogora huyo akome kuwasiliana mara kwa mara na wapenzi wake wa zamani, pia alimtaka amtwae rasmi na kumfanya wake wa halali kwa kula yamini ya ndoa.

Akitumia mitandao yake ya kijamii, Ronaldo alipakia picha aliyopigwa pamoja na Georgina wakishikilia picha ya matokeo ya vipimo vya ujauzito wa kipusa huyo aliyewahi kuwa yaya na mhudumu wa dukani.

“Furaha isiyo kifani kwamba tunatarajia mapacha. Mioyo yetu imejaa mapenzi na tunasubiri kwa hamu kubwa kukutana nanyi,” akaandika Ronaldo.

“Hamu yangu ya kuwa mama kwa mara nyingine ni kubwa kuliko kitu chochote kingine. Sitakomea kwa hawa wawili ninaotarajia. Nina kiu ya kujaza dunia,” akaandika Georgina.

Maria Dolores dos Santos Aveiro ambaye ni mama yake Ronaldo, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza mwanasoka huyo kwa kazi nzuri anayofanya chumbani.

Mama aliandika kwenye Instagram: “Naomba wajukuu hawa watoke wakiwa na afya njema. Hilo ndilo kubwa zaidi kwa sasa.”Ronaldo alikutana na Georgina kwa mara ya kwanza mnamo 2016 kichuna huyo akiwa muuzaji wa duka la kuuza bidhaa za Gucci jijini Madrid, Uhispania kwa malipo ya Sh1,500 kwa saa moja.

Tangu wakati huo, Georgina amefuatana na Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa taji la Ballon d’Or kuanzia Uhispania hadi Italia na Uingereza baada ya fowadi huyo kuondoka Real Madrid na kutua Juventus kabla ya kurejea Man-United.

Akihojiwa na wanahabari mwezi uliopita, Georgina alifichua kwamba anatazamia kwa hamu kubwa siku ambapo Ronaldo atamvisha pete ya ndoa.

“Suala la kufunga pingu za maisha sasa linategemea Ronaldo. Natamani sana siku hiyo ije upesi,” akasema.

Kwa upande wake, Ronaldo alikiri kwamba kuitwa baba humletea furaha zaidi kuliko tija na fahari ambayo amejivunia kwa kunyanyua mataji ya kila sampuli katika ulingo wa soka nchini Uingereza, Uhispania, Italia na Ureno.

Dolores, 66, amekuwa akimsifia Georgina mara kwa mara kutokana na jinsi anavyomtunza Ronaldo pamoja na kumpa fursa maridhawa ya kuzamia taaluma yake ya usogora.

Alishikilia kwamba kati ya warembo wote waliowahi kumburudisha Ronaldo, hakuna anayemvutia pia kitabia na kimwonekano kuliko Georgina.

You can share this post!

UDAKU: Binti wa Guardiola abaki kwa mataa Dele Alli...

Askofu Anyolo amshukuru Papa kumkweza

T L