Habari Mseto

Daktari motoni mahakama kusimuliwa alivyotekeleza mauaji

August 28th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

KESI dhidi ya daktari anayeshtakiwa kumuua mumewe miaka 13 ilianza kusikizwa Jumanne katika mahakama ya Citi, Nairobi.

Akitoa ushahidi Dkt Jane Wasike aliyefanyia upasuaji mwili wa Yogesh Sapra alisema kifo cha mfanyabiashara huyo kilitokana na majeraha ya kudungwa kwa kisu.

“Marehemu alikuwa na vidonda vitatu kwenye tumbo, kifuani na  kwenye mbavu,” hakimu mkuu katika mahakama ya Citi Bi Roseline Onganyo alifashamishwa na Dkt Wasike

Daktari huyo alisema kutokana na majeraha aliyopata, Bw Sapra alipatwa na magonjwa mengine na kupelekea kufariki kwake.

Dkt Wasike alisema alifanyia upasuaji mwili huo mnamo Septemba 10, 2005 baada ya kutambuliwa na nduguye Kuldip Sapra na Bi Sheetal Sapra.

Akiongozwa kutoa ushahidi na wakili wa Serikali Bw Edwin Okello, Dkt Wasike alisema  marehemu alikuwa na umri wa miaka 47 alipoaga.

Mahakama ilifahamishwa kuwa mapafu yalikuwa na maji mengi na alikuwa na matatizo ya kuenda choo.

Dkt Zephania  Kamau aliyempima Dkt Nisha Sapra anayeshtakiwa kumuua mumewe alikuwa mwenye akili timamu. Dkt Kamau alisema alimpima akili Septemba 23, 2005.

“Mshtakiwa alifikishwa katika afisi yangu na afisa anayechunguza kesi hiii. Nilimpima nikaona yuko na akili timamu,” alisema  Dkt Kamau.

Mshtakiwa amekanusha shtaka la kumuua Yogesh Sapra mnamo Agosti 5, 2005.

Dkt Sapra ambaye ni daktari wa kung’oa meno amekanusha shtaka na yuko nje kwa dhamana.

Kesi hiyo itaendelea Septemba 3, 2015.