DARUBINI YA UKWELI: Ripoti ya TJRC inarejelea Vita vya Shifta

DARUBINI YA UKWELI: Ripoti ya TJRC inarejelea Vita vya Shifta

BAADHI ya wanablogu wa mrengo wa Azimio-One Kenya wamekuwa wakisambaza ukurasa wanaodai kuwa wa ripoti ya Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano (TJRC).

Kwenye ukurasa huo (Uk 103) wa ripoti hiyo, una maelezo yanayodai kuwa Mgombea-Mwenza Naibu Rais William Ruto, Bw Rigathi Gachagua alikuwa akipata maagizo kutoka kwa marehemu Daniel Moi kusimamia vitendo vya kikatili katika eneo la Molo.

Ukweli ni kuwa, ijapokuwa ripoti hiyo imerejelea kwa kina ghasia hizo, ukurasa 103 unarejelea vita kati ya Kenya na Somalia katika miaka ya sitini, maarufu kama “Vita vya Shifta.”

Uamuzi: Ukurasa 103 wa ripoti ya TJRC haumtaji kwa vyovyote Rigathi Gachagua, bali unarejelea Vita vya Shifta kati ya Kenya na Somalia

  • Tags

You can share this post!

Oparanya akaripia Mudavadi, Weta’ kuhusu maendeleo

Wamiliki hoteli waelezea hofu kuhusu Covid-19

T L