Dawa mpya yathibitishwa kuwa na uwezo wa kupunguza makali ya HIV

Dawa mpya yathibitishwa kuwa na uwezo wa kupunguza makali ya HIV

Na LEONARD ONYANGO

WAATHIRIWA wa HIV huenda wakapunguziwa usumbufu wa kumeza tembe za kupunguza makali ya virusi hivyo (ARVs) kila siku baada ya dawa inayodungwa kwa sindano kila baada ya miezi miwili kuthibitishwa kuwa na uwezo.

Dawa hiyo iliyo na mchanganyiko wa tembe za cabotegravir na rilpivirine imethibitishwa kuwa ina uwezo wa kupunguza makali ya HIV mwilini sawa na ARVs.Serikali ya Scotland tayari imeidhinisha matumizi ya dawa hiyo inayodungwa kwa sindano badala ya kumeza tembe za kila siku.

Wataalamu wanasema kuwa sindano hiyo itasaidia pakubwa kupunguza visa vya unyanyapaa vinavyoambatana na kumeza tembe kila wakati.Dawa hiyo ilianza kufanyiwa majaribio nchini Uganda wiki iliyopita.

Majaribio pia yanatarajiwa kufanyika humu nchini na Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka huu.

 

You can share this post!

DKT FLO: Mbinu asili za kuzuia kisukari ni salama?

Maradhi ya Trakoma yanapofusha maelfu maeneo kame

F M