Habari Mseto

DCI aliyebaka mwanamke kituoni aachiliwa kwa bondi ya Sh500,000

June 11th, 2020 1 min read

NA GEORGE MUNENE

Afisa wa ngazi ya juu katika kitengo cha DCI ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka mwanamke mmoja aliyekuwa chini ya ulinzi wake.

Jerevasio Njeru anasemekana kutenda kitendo hicho katika kituo cha polisi cha Manyatta hapo Mei 31 2020.

Mwanamke huyo mwenye miaka 42 anasemekana alibakwa akiwa amezuiliwa kituoni kutokana na kosa la wizi..

Alishtakiwa kwa mara ya pili kwa kosa la kunajisi mwanamke huyo kwa kumshika sehemu zake za siri.

Njeru alifika kortini chini ya ulinzi mkubwa na kupelekwa kizimbani. Alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu Maxwell Giche na kuachiliwa kwa bondi ya Sh500,000.